Maandishi ya kauli hiyo yanasema hivi:
"Imepita miaka 46 tangu kutekwa nyara Imam Sadr huko Libya, na juhudi za kumrudisha tena yeye na masahaba wake 2 hazijazaa matunda."
Nafasi iliyowazi ya Kiongozi wa Upinzani / Muqawamah inahisiwa zaidi Siku hizi nchini Lebanon na katika eneo hili la Mashariki ya Kati.
Zaidi ya miongo mitano iliyopita, aliitaja Israel kuwa ni uovu mtupu na akazingatia hatari yake kuliko kitu kingine chochote katika eneo la Mashariki ya Kati na Dunia nzima.
Imam Musa Sadr aliichukulia Israel si tu kuwa ni adui wa Wapalestina, bali pia ni adui wa Mwanadamu na Ubinadamu. Sasa kwa vile Israel imeonyesha sura yake halisi zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika mwaka huu mmoja, na imeonyesha kuwa iko tayari kuharibu maisha ya Watoto wasio na ulinzi wa Kipalestina, pamoja na Wanawake na Wanaume, kinyume na desturi na maadili yote ya Mwanadamu, hilo linadhihirisha tafsiri na mitazamo ya Imam Mussa Sadr kuhusu hatari hiyo na kuifanya mitizamo yake iwe ni yenye kueleweka zaidi.
Tunatumai kuwa kupitia juhudi za wale wote wanaoweza kufanya jambo, fumbo hili tata litaweza kutatuliwa".